Mgeni aishiye pamoja nawe atakuwa kama mzaliwa kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Hesabu 10:32 - Swahili Revised Union Version Isitoshe, ukienda pamoja nasi, naam, mema yote ambayo BWANA atatutendea, nawe tutakutendea vivyo hivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena ukiandamana nasi chochote chema atakachotutendea Mwenyezi-Mungu, ndicho utakachotendewa nawe pia.” Biblia Habari Njema - BHND Tena ukiandamana nasi chochote chema atakachotutendea Mwenyezi-Mungu, ndicho utakachotendewa nawe pia.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena ukiandamana nasi chochote chema atakachotutendea Mwenyezi-Mungu, ndicho utakachotendewa nawe pia.” Neno: Bibilia Takatifu Ikiwa utafuatana nasi, tutashirikiana nawe mema yoyote tutakayopewa na Mwenyezi Mungu.” Neno: Maandiko Matakatifu Ikiwa utafuatana nasi, tutashirikiana nawe mema yoyote tutakayopewa na bwana.” BIBLIA KISWAHILI Isitoshe, ukienda pamoja nasi, naam, mema yote ambayo BWANA atatutendea, nawe tutakutendea vivyo hivyo. |
Mgeni aishiye pamoja nawe atakuwa kama mzaliwa kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.
hilo tuliloliona na kulisikia, tunawahubiria na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
Hao wana wa Mkeni, huyo shemeji yake Musa, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao.
Basi Heberi, Mkeni, alikuwa amejitenga na Wakeni, yaani na wana wa Hobabu, shemeji yake Musa, akaipiga hema yake mbali penye mwaloni ulioko Saananimu, karibu na Kedeshi.
Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha zake, Haya! Na twende tukavuke ngomeni mwa hao wasiotahiriwa; yamkini BWANA atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia BWANA asiokoe, kama ni kwa wengi au kama ni kwa wachache.