Hii ndiyo nakala ya waraka waliyompelekea mfalme Artashasta; Watumishi wako, watu walio ng'ambo ya Mto; wakadhalika.
Ezra 7:11 - Swahili Revised Union Version Basi hii ndiyo nakala ya barua, ambayo mfalme Artashasta alimpa Ezra, kuhani, mwandishi, mjuzi wa amri za BWANA, na sheria zake alizowapa Waisraeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ifuatayo ni barua ambayo Artashasta alimpa Ezra, kuhani na mwandishi, na mwenye ujuzi katika amri na masharti ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa watu wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Ifuatayo ni barua ambayo Artashasta alimpa Ezra, kuhani na mwandishi, na mwenye ujuzi katika amri na masharti ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa watu wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ifuatayo ni barua ambayo Artashasta alimpa Ezra, kuhani na mwandishi, na mwenye ujuzi katika amri na masharti ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa watu wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Hii ni nakala ya barua ambayo Mfalme Artashasta alimpa Ezra aliyekuwa kuhani na mwalimu, mtu aliyeelimika katika mambo kuhusu maagizo na amri za Mwenyezi Mungu kwa Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Hii ni nakala ya barua ambayo Mfalme Artashasta alikuwa amempa Ezra aliyekuwa kuhani na mwalimu, mtu aliyeelimika katika mambo yahusuyo maagizo na amri za bwana kwa Israeli. BIBLIA KISWAHILI Basi hii ndiyo nakala ya barua, ambayo mfalme Artashasta alimpa Ezra, kuhani, mwandishi, mjuzi wa amri za BWANA, na sheria zake alizowapa Waisraeli. |
Hii ndiyo nakala ya waraka waliyompelekea mfalme Artashasta; Watumishi wako, watu walio ng'ambo ya Mto; wakadhalika.
Hii ndiyo nakala ya waraka ambao; Tatenai, Mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng'ambo ya Mto; walimtumia mfalme Dario.
Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.
Artashasta, mfalme wa wafalme, kwa Ezra, kuhani, mwandishi wa Torati ya Mungu wa mbinguni, wasalamu; na kadhalika.
Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri watunza hazina wote, walio ng'ambo ya Mto, ya kwamba, kila neno ambalo Ezra, kuhani, mwandishi wa Torati ya Mungu wa mbinguni, atalitaka kwenu, na litendeke kwa bidii nyingi,
huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika Sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa BWANA, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa BWANA, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.