kwa sababu hawakuitii sauti ya BWANA, Mungu wao, bali waliyavunja maagano yake, mambo yote ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwaamuru, wasikubali kuyasikiliza, wala kuyatenda.
Danieli 9:10 - Swahili Revised Union Version wala hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tulikataa kukusikiliza, ee Bwana, Mungu wetu; hatukuishi kulingana na sheria zako ulizotupa kwa njia ya watumishi wako manabii. Biblia Habari Njema - BHND Tulikataa kukusikiliza, ee Bwana, Mungu wetu; hatukuishi kulingana na sheria zako ulizotupa kwa njia ya watumishi wako manabii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tulikataa kukusikiliza, ee Bwana, Mungu wetu; hatukuishi kulingana na sheria zako ulizotupa kwa njia ya watumishi wako manabii. Neno: Bibilia Takatifu Hatukumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, wala kuzishika sheria alizotupatia kupitia kwa watumishi wake, manabii. Neno: Maandiko Matakatifu Hatukumtii bwana Mwenyezi Mungu wetu wala kuzishika sheria alizotupa kupitia kwa watumishi wake manabii. Swahili Roehl Bible 1937 Hatukuisikia sauti ya Bwana Mungu wetu, tuyafuate Maonyo yake, aliyotupa mikononi mwa watumishi wake wafumbuaji, tuyaangalie. |
kwa sababu hawakuitii sauti ya BWANA, Mungu wao, bali waliyavunja maagano yake, mambo yote ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwaamuru, wasikubali kuyasikiliza, wala kuyatenda.
Ndipo utakapowaambia, Ni kwa sababu baba zenu wameniacha mimi, asema BWANA, na kuwafuata miungu mingine, na kuwatumikia, na kuwaabudu, wakaniacha mimi, wasiishike torati yangu;
nao wakaingia, wakaimiliki; lakini hawakuitii sauti yako, wala hawakuenda katika sheria yako; hawakutenda neno lolote katika haya uliyowaagiza wayatende; basi, kwa sababu hii umeleta juu yao mabaya haya yote;
wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,