Danieli 9:11 - Swahili Revised Union Version11 Naam, Israeli wote wameivunja sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na kiapo kile kilioandikwa katika Sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema11 Waisraeli wote wameiasi sheria yako, wamekuacha wakakataa kukutii. Kwa sababu tumekukosea, tumemwagiwa laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Mose, mtumishi wako. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND11 Waisraeli wote wameiasi sheria yako, wamekuacha wakakataa kukutii. Kwa sababu tumekukosea, tumemwagiwa laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Mose, mtumishi wako. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza11 Waisraeli wote wameiasi sheria yako, wamekuacha wakakataa kukutii. Kwa sababu tumekukosea, tumemwagiwa laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Mose, mtumishi wako. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu11 Israeli wote wamekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii. “Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu11 Israeli yote imekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii. “Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako. Tazama suraSwahili Roehl Bible 193711 Waisiraeli wote wakapita tu penye Maonyo yako, wakaenda zao pasipo kuisikia sauti yako; kwa sababu hiyo tukamwagiwa kiapizo, kikatupata nacho kiapo kilichoandikwa katika Maonyo ya Mose, mtumwa wake Mungu, kwani tulimkosea. Tazama sura |