Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.
Danieli 6:19 - Swahili Revised Union Version Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alfajiri na mapema, mfalme Dario aliamka, akaenda kwa haraka kwenye pango la simba. Biblia Habari Njema - BHND Alfajiri na mapema, mfalme Dario aliamka, akaenda kwa haraka kwenye pango la simba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alfajiri na mapema, mfalme Dario aliamka, akaenda kwa haraka kwenye pango la simba. Neno: Bibilia Takatifu Asubuhi na mapema, mfalme akaondoka na kuharakisha kwenda kwenye tundu la simba. Neno: Maandiko Matakatifu Asubuhi na mapema, mfalme akaondoka na kuharakisha kwenda kwenye tundu la simba. Swahili Roehl Bible 1937 Asubuhi mapema kulipopambazuka, mfalme akaondoka, akaenda na kulikimbilia lile pango la simba. |
Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.
Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?
Na sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
Na alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;
sikuona raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.