Ndipo Bathsheba akainama kifudifudi, akamsujudia mfalme, akasema, Bwana wangu mfalme Daudi na aishi milele.
Danieli 3:9 - Swahili Revised Union Version Wakajibu, wakamwambia mfalme Nebukadneza, Ee mfalme, uishi milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Uishi, ee mfalme! Biblia Habari Njema - BHND “Uishi, ee mfalme! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Uishi, ee mfalme! Neno: Bibilia Takatifu Wakamwambia Mfalme Nebukadneza, “Ee mfalme, uishi milele! Neno: Maandiko Matakatifu Wakamwambia Mfalme Nebukadneza, “Ee mfalme, uishi milele! Swahili Roehl Bible 1937 wakamwambia mfalme Nebukadinesari hivyo: E mfalme, na uwe mwenye uzima kale na kale! |
Ndipo Bathsheba akainama kifudifudi, akamsujudia mfalme, akasema, Bwana wangu mfalme Daudi na aishi milele.
Ndipo hao Wakaldayo wakamwambia mfalme, kwa lugha ya Kiaramu, Ee Mfalme, uishi milele; tuambie sisi watumishi wako ile ndoto, nasi tutakuonesha tafsiri yake.
Basi malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike.
Basi wale mawaziri na viongozi wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.