Danieli 5:10 - Swahili Revised Union Version10 Basi malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema10 Kutokana na kelele za mfalme na wakuu wake, mama mfalme aliingia ukumbini mwa karamu, akasema, “Uishi, ee mfalme! Si lazima mawazo yako yakufadhaishe na kubadilika rangi yako. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND10 Kutokana na kelele za mfalme na wakuu wake, mama mfalme aliingia ukumbini mwa karamu, akasema, “Uishi, ee mfalme! Si lazima mawazo yako yakufadhaishe na kubadilika rangi yako. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza10 Kutokana na kelele za mfalme na wakuu wake, mama mfalme aliingia ukumbini mwa karamu, akasema, “Uishi, ee mfalme! Si lazima mawazo yako yakufadhaishe na kubadilika rangi yako. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu10 Malkia aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake, alikuja katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele! Usishtuke! Usibadilike rangi hivyo! Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu10 Malkia aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake, alikuja katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele! Usishtuke! Usibadilike rangi kiasi hicho! Tazama suraSwahili Roehl Bible 193710 Kwa ajili ya hayo maneno ya mfalme na ya wakuu wake mamake mfalme akaja mle chumbani, walimonywea, kisha mamake mfalme akasema kwamba: Wewe mfalme na uwe mwenye uzima kale na kale! Mawazo yako yasikustushe, wala uso wako usiwe mwingine! Tazama sura |