Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Danieli 2:6 - Swahili Revised Union Version

Bali kama mkinionesha ile ndoto na tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionesheni ile ndoto na tafsiri yake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lakini mkiniambia hiyo ndoto na maana yake, nitawapa zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi, nijulisheni ndoto hiyo na maana yake!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lakini mkiniambia hiyo ndoto na maana yake, nitawapa zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi, nijulisheni ndoto hiyo na maana yake!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lakini mkiniambia hiyo ndoto na maana yake, nitawapa zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi, nijulisheni ndoto hiyo na maana yake!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuifasiri, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuielezea, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.”

Tazama sura

Swahili Roehl Bible 1937

Lakini mkiweza kuieleza hiyo ndoto na maana yake, mtapata matunzo na vipaji na macheo makuu mbele yangu. Kwa hiyo ielezeni ndoto na maana yake!

Tazama sura
Tafsiri zingine



Danieli 2:6
8 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya utawala wote wa Babeli, na kuwa mtawala mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.


Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.


Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme.


maana nitakutunukia heshima kubwa sana, na neno lolote utakaloniomba nitalitenda; basi njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa.


Balaki akamwambia Balaamu, Je! Mimi sikutuma watu kwako kwa bidii ili kukuita? Mbona hukunijia? Je! Siwezi mimi kukufanyizia heshima nyingi?


Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.


Basi sasa kimbilia mahali pako; niliazimu kukuheshimu sana; lakini, tazama, BWANA amekuzuilia heshima.