utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema, Jinsi mdhalimu alivyokoma; Jinsi ulivyokoma mji ule wenye ujeuri!
Danieli 2:32 - Swahili Revised Union Version Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kichwa cha sanamu hiyo kilikuwa cha dhahabu safi, kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha na tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba. Biblia Habari Njema - BHND Kichwa cha sanamu hiyo kilikuwa cha dhahabu safi, kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha na tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kichwa cha sanamu hiyo kilikuwa cha dhahabu safi, kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha na tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba. Neno: Bibilia Takatifu Kichwa cha sanamu hiyo kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi; kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha; tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba; Neno: Maandiko Matakatifu Kichwa cha ile sanamu kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi, kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha, tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba, Swahili Roehl Bible 1937 Hicho kinyago kichwa chake kilikuwa cha dhahabu tupu, kifua chake na mikono yake ilikuwa ya fedha, tumbo lake na viuno vyake vilikuwa vya shaba, |
utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema, Jinsi mdhalimu alivyokoma; Jinsi ulivyokoma mji ule wenye ujeuri!
Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.
ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.
Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe makao yangu ya kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?
Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.