Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 2:31 - Swahili Revised Union Version

31 Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa la kutisha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 “Katika ndoto yako, ee mfalme, uliona sanamu kubwa, yenye nguvu na iliyongaa sana, imesimama mbele yako. Sanamu hiyo ilikuwa ya kutisha mno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 “Katika ndoto yako, ee mfalme, uliona sanamu kubwa, yenye nguvu na iliyongaa sana, imesimama mbele yako. Sanamu hiyo ilikuwa ya kutisha mno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 “Katika ndoto yako, ee mfalme, uliona sanamu kubwa, yenye nguvu na iliyong'aa sana, imesimama mbele yako. Sanamu hiyo ilikuwa ya kutisha mno.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 “Ee mfalme, ulitazama, na mbele yako ilisimama sanamu kubwa mno, iliyong’aa kupita kiasi na yenye kutisha kwa mwonekano wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 “Ee mfalme, ulitazama, na mbele yako ilisimama sanamu kubwa, kubwa mno kupita kiasi, sanamu iliyong’aa na kutisha kwa kuonekana kwake.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

31 Wewe mfalme ulikuwa ukiota, mara ukaona kinyago kimoja. Kinyago hicho kilikuwa kikubwa sana, kikametuka kabisa, kikasimama mbele yako, kikatia woga kwa kutazamwa tu.

Tazama sura Nakili




Danieli 2:31
11 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;


basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako.


Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme.


Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;


Nebukadneza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.


Basi wakati huo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.


Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe.


Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,


Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo