Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Danieli 2:1 - Swahili Revised Union Version

Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadneza, Nebukadneza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, akatokwa na usingizi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mnamo mwaka wa pili wa utawala wake, mfalme Nebukadneza aliota ndoto, akawa na wasiwasi sana rohoni hata usingizi ukamtoweka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mnamo mwaka wa pili wa utawala wake, mfalme Nebukadneza aliota ndoto, akawa na wasiwasi sana rohoni hata usingizi ukamtoweka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mnamo mwaka wa pili wa utawala wake, mfalme Nebukadneza aliota ndoto, akawa na wasiwasi sana rohoni hata usingizi ukamtoweka.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala.

Tazama sura

Swahili Roehl Bible 1937

Katika mwaka wa pili wa ufalme wake mfalme Nebukadinesari akaota ndoto, zikamhangaisha rohoni, kwa hiyo usingizi ukampotelea.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Danieli 2:1
14 Marejeleo ya Msalaba  

Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha kumbukumbu nacho kikasomwa mbele ya mfalme.


Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, katika habari za watu wote wa Yuda; katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda mwaka ule ndio mwaka wa kwanza wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli;


Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake.


Mimi nimeona vema kutangaza habari za ishara na maajabu, aliyonitendea Mungu aliye juu.


Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.


Ndipo mfalme Belshaza akahangaika sana, uso wake ukambadilika, na wakuu wake wakaona fadhaa.


Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.


Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli alipata ndoto, na maono kichwani nwake, akiwa kitandani mwake; kisha akaiandika hiyo ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.


Basi, mimi Danieli, roho yangu ilihuzunika ndani yangu, na hayo maono ya kichwa changu yakanifadhaisha.