Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Danieli 11:3 - Swahili Revised Union Version

Na mfalme hodari atasimama, atakayetawala kwa uwezo mkuu, na kutenda apendavyo.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kisha atatokea mfalme hodari atakayetawala eneo kubwa na kufanya atakavyopenda.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kisha atatokea mfalme hodari atakayetawala eneo kubwa na kufanya atakavyopenda.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kisha atatokea mfalme hodari atakayetawala eneo kubwa na kufanya atakavyopenda.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ndipo mfalme mwenye nguvu atatokea, atakayetawala kwa nguvu nyingi, na kufanya anavyopenda.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ndipo mfalme mwenye nguvu atatokea, ambaye atatawala kwa nguvu nyingi na kufanya anavyopenda.

Tazama sura

Swahili Roehl Bible 1937

Kisha ataondokea mfalme mwenye nguvu za kupiga vita, naye atatawala kwa uwezo mwingi, atafanya yatakayompendeza.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Danieli 11:3
10 Marejeleo ya Msalaba  

Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, wala hapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.


Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa miungu, naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa yatafanyika.


na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?


na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.


Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.


Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Ugiriki; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.


na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.


Mungu naye akishuhudia pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.


Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.