Danieli 10:18 - Swahili Revised Union Version Kisha mmoja mfano wa mwanadamu akanigusa tena, akanitia nguvu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Yule mmoja aliyeonekana kama mwanaadamu akanigusa kwa mara nyingine, akanitia nguvu. Biblia Habari Njema - BHND “Yule mmoja aliyeonekana kama mwanaadamu akanigusa kwa mara nyingine, akanitia nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Yule mmoja aliyeonekana kama mwanaadamu akanigusa kwa mara nyingine, akanitia nguvu. Neno: Bibilia Takatifu Tena yule aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa na kunitia nguvu. Neno: Maandiko Matakatifu Tena yule aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa na kunitia nguvu. Swahili Roehl Bible 1937 Ndipo, yeye aliyefanana na mtu aliponigusa tena, akanitia nguvu, |
Na kumbe, mmoja mfano wa wanadamu akanigusa midomo yangu; ndipo nikafumbua kinywa changu, nikanena, nikamwambia yeye aliyesimama karibu nami, Ee Bwana wangu, kwa sababu ya maono haya huzuni zangu zimenipata tena; hata sikubakia na nguvu.
Ikawa mimi, naam, mimi Danieli, nilipoyaona maono hayo, nilitafuta kuyafahamu, na tazama, alisimama mbele yangu mmoja mfano wa mwanadamu.
Basi alipokuwa akisema nami, nilishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.
lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Baada ya kukaa huko kwa siku kadhaa akaondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi.
awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.
mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
Daudi akaona ya kwamba Sauli ametoka nje ili kutafuta roho yake; naye Daudi akawako katika nyika ya Zifu, huko Horeshi.