Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;
Danieli 10:10 - Swahili Revised Union Version Na tazama, mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na viganja vya mikono yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo, mkono ukanigusa, ukanisimamisha, na kuimarisha miguu na mikono yangu. Biblia Habari Njema - BHND Hapo, mkono ukanigusa, ukanisimamisha, na kuimarisha miguu na mikono yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo, mkono ukanigusa, ukanisimamisha, na kuimarisha miguu na mikono yangu. Neno: Bibilia Takatifu Mkono ulinigusa, ukaninyanyua na kuniweka magotini, mikono yangu ikishika chini, huku nikiwa bado ninatetemeka. Neno: Maandiko Matakatifu Mkono ulinigusa, ukaninyanyua, na kuniweka nikipiga magoti na mikono yangu ikashika chini, huku nikiwa bado ninatetemeka. Swahili Roehl Bible 1937 Mara mkono ukanigusa, ukanisaidia kuinuka, kwa kuwa magoti na viganja vya mikono vilikuwa vikitetemeka. |
Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;
Na kumbe, mmoja mfano wa wanadamu akanigusa midomo yangu; ndipo nikafumbua kinywa changu, nikanena, nikamwambia yeye aliyesimama karibu nami, Ee Bwana wangu, kwa sababu ya maono haya huzuni zangu zimenipata tena; hata sikubakia na nguvu.
Basi alipokuwa akisema nami, nilishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.
naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,