Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 10:11 - Swahili Revised Union Version

11 Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame wima; maana nimetumwa kwako sasa. Na aliponiambia neno hili, nilisimama nikitetemeka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Akaniambia, ‘Danieli, wewe unayependwa sana, simama wima usikilize kwa makini maneno nitakayosema, maana nimetumwa kwako.’ Alipokuwa akiniambia maneno haya, mimi nilisimama nikitetemeka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Akaniambia, ‘Danieli, wewe unayependwa sana, simama wima usikilize kwa makini maneno nitakayosema, maana nimetumwa kwako.’ Alipokuwa akiniambia maneno haya, mimi nilisimama nikitetemeka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Akaniambia, ‘Danieli, wewe unayependwa sana, simama wima usikilize kwa makini maneno nitakayosema, maana nimetumwa kwako.’ Alipokuwa akiniambia maneno haya, mimi nilisimama nikitetemeka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayoenda kunena nawe; simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Aliponiambia haya, nikasimama nikitetemeka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayokwenda kunena nawe sasa; simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Naye aliponiambia haya, nikasimama nikitetemeka.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

11 Kisha akaniambia: Danieli, ndiwe mtu wa kupendezwa naye; yatambue hayo maneno, mimi nitakayokuambia, ukisimama hapohapo, unaposimama! kwani nimetumwa kwako. Aliponiambia neno hili, nikainuka na kutetemeka.

Tazama sura Nakili




Danieli 10:11
15 Marejeleo ya Msalaba  

Moyo wangu hutetemeka kwa hayo pia, Nao huruka kutoka mahali pake.


Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.


Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu.


wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU.


Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe.


Akasema, Ee mtu upendwaye sana, usiogope; amani na iwe kwako, uwe na nguvu, naam, uwe na nguvu. Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu; kwa maana umenitia nguvu.


Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia.


Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingiwa na hofu na mshangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa. [


Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.


Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)


Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;


Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo