Amosi 8:12 - Swahili Revised Union Version Nao watatangatanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huku na huko, kulitafuta neno la BWANA, wasilione. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu watatangatanga kutoka bahari hata bahari, kutoka upande wa kaskazini mpaka mashariki. Watakimbia huko na huko wakitafuta neno la Mwenyezi-Mungu, lakini hawatalipata. Biblia Habari Njema - BHND Watu watatangatanga kutoka bahari hata bahari, kutoka upande wa kaskazini mpaka mashariki. Watakimbia huko na huko wakitafuta neno la Mwenyezi-Mungu, lakini hawatalipata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu watatangatanga kutoka bahari hata bahari, kutoka upande wa kaskazini mpaka mashariki. Watakimbia huko na huko wakitafuta neno la Mwenyezi-Mungu, lakini hawatalipata. Neno: Bibilia Takatifu Wanaume watayumbayumba kutoka bahari hadi bahari na kutangatanga kutoka kaskazini mpaka mashariki, wakitafuta neno la Mwenyezi Mungu, lakini hawatalipata. Neno: Maandiko Matakatifu Wanaume watayumbayumba kutoka bahari hadi bahari na kutangatanga kutoka kaskazini mpaka mashariki, wakitafuta neno la bwana, lakini hawatalipata. BIBLIA KISWAHILI Nao watatangatanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huku na huko, kulitafuta neno la BWANA, wasilione. |
Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mmekuja kuniuliza neno? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.
Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.
Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.
Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe wamtafute BWANA; lakini hawatamwona; amejitenga nao.
Basi, mtoto Samweli akamtumikia BWANA mbele ya Eli. Na neno la BWANA lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.