Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu zilinifikia. Kisha akawatolea Simeoni kwao.
3 Yohana 1:14 - Swahili Revised Union Version Lakini natarajia kukuona karibuni, nasi tutasema uso kwa uso. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana. Biblia Habari Njema - BHND Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana. Neno: Bibilia Takatifu Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana. Neno: Maandiko Matakatifu Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana. BIBLIA KISWAHILI Lakini natarajia kukuona karibuni, nasi tutasema uso kwa uso. |
Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu zilinifikia. Kisha akawatolea Simeoni kwao.
Mfalme Nebukadneza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.
Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi.
Amani na iwe kwa ndugu, na upendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.
Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini natarajia kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.