Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




3 Yohana 1:10 - Swahili Revised Union Version

Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuza nje ya kanisa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuza nje ya kanisa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuza nje ya kanisa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hivyo nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke miongoni mwa waumini.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hivyo kama nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke miongoni mwa kundi la waumini.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



3 Yohana 1:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.


Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.


Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.


Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.


Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kukubaliana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi.


Siku zile akasimama Petro kati ya hao ndugu (jumla ya majina ilikuwa mia moja na ishirini), akasema,


Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia;


Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.


Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.


Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.


Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini natarajia kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.


Maana nilifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.


Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao,