Na mama yake yule mtoto akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Basi akaondoka, akamfuata.
2 Wafalme 6:3 - Swahili Revised Union Version Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mmoja wao akamwomba akisema, “Tafadhali uwe radhi uende na watumishi wako.” Naye akajibu, “Nitakwenda.” Biblia Habari Njema - BHND Mmoja wao akamwomba akisema, “Tafadhali uwe radhi uende na watumishi wako.” Naye akajibu, “Nitakwenda.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mmoja wao akamwomba akisema, “Tafadhali uwe radhi uende na watumishi wako.” Naye akajibu, “Nitakwenda.” Neno: Bibilia Takatifu Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?” Al-Yasa akajibu, “Nitakuja.” Neno: Maandiko Matakatifu Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?” Al-Yasa akajibu, “Nitakuja.” BIBLIA KISWAHILI Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda. |
Na mama yake yule mtoto akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Basi akaondoka, akamfuata.
Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamsihi, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakatangulia mbele yake wakiwa wameyabeba.
Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni.
Basi wakaketi, wakala na kunywa wote wawili pamoja; kisha baba yake mwanamke akamwambia huyo mtu, Uwe radhi, tafadhali, ukae usiku kucha, na moyo wako na ufurahi.
Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi.