2 Wafalme 4:3 - Swahili Revised Union Version Akasema, Nenda, ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime vichache. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Elisha akamwambia, “Nenda kwa jirani zako uazime vyombo vitupu vingi kadiri utakavyopata. Biblia Habari Njema - BHND Elisha akamwambia, “Nenda kwa jirani zako uazime vyombo vitupu vingi kadiri utakavyopata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Elisha akamwambia, “Nenda kwa jirani zako uazime vyombo vitupu vingi kadiri utakavyopata. Neno: Bibilia Takatifu Al-Yasa akasema, “Zunguka kwa majirani zako wote ukaombe vyombo vitupu. Usiombe vichache. Neno: Maandiko Matakatifu Al-Yasa akasema, “Zunguka kwa majirani zako wote ukaombe vyombo vitupu. Usiombe vichache. BIBLIA KISWAHILI Akasema, Nenda, ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime vichache. |
Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.
Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.
Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.
Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.