Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

2 Wafalme 22:1 - Swahili Revised Union Version

Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Yedida, binti Adaya wa Bozkathi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala huko Yerusalemu, akatawala kwa miaka thelathini na mmoja. Mama yake alikuwa Yedida, binti Adaya, mkazi wa mji wa Boskathi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala huko Yerusalemu, akatawala kwa miaka thelathini na mmoja. Mama yake alikuwa Yedida, binti Adaya, mkazi wa mji wa Boskathi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala huko Yerusalemu, akatawala kwa miaka thelathini na mmoja. Mama yake alikuwa Yedida, binti Adaya, mkazi wa mji wa Boskathi.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Yosia alikuwa na umri wa miaka nane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na moja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Yedida, binti Adaya wa Bozkathi.

Tazama sura
Tafsiri zingine

2 Wafalme 22:1
14 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la BWANA akasema, Ee madhabahu, madhabahu, BWANA asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawatambika makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.

Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala.

Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na mitano katika Yerusalemu, na jina la mamaye aliitwa Hefziba.

Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliomfitinia mfalme Amoni, watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme mahali pake.

Akazikwa kaburini mwake katika bustani ya Uza. Na Yosia mwanawe akatawala mahali pake.

Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi.

Ole wako, nchi, iwapo mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi!

Nami nitawapa watoto kuwamiliki, na watoto wachanga kuwatawala.

ambaye neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa kutawala kwake.

Na kama yeye huyo akizaa mwana, naye ameona dhambi zote za baba yake alizozitenda, akaogopa, asifanye neno lolote kama hayo;

Neno la BWANA lililomjia Sefania, mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia; katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda.

Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;

Lakishi, Bozkathi, Egloni;