Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
2 Timotheo 2:5 - Swahili Revised Union Version Hata mwanariadha hapewi taji, asiposhindana kwa kufuata sheria. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo. Biblia Habari Njema - BHND Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo. Neno: Bibilia Takatifu Vivyo hivyo, mwanariadha hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano. Neno: Maandiko Matakatifu Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano. BIBLIA KISWAHILI Hata mwanariadha hapewi taji, asiposhindana kwa kufuata sheria. |
Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema.
Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.
Umemfanya mdogo kwa muda kuliko malaika, Umemvika taji la utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo kwa muda kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji la utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.
ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao hutupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,
Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti niliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wameikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji la dhahabu.