Basi, wale askari wakamchukua Paulo kama walivyoamriwa, wakampeleka hadi Antipatri usiku;
2 Timotheo 2:3 - Swahili Revised Union Version Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Al-Masihi Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Al-Masihi Isa. BIBLIA KISWAHILI Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu. |
Basi, wale askari wakamchukua Paulo kama walivyoamriwa, wakampeleka hadi Antipatri usiku;
Ni askari gani aendaye vitani wakati wowote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?
Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.
Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyonenwa awali juu yako, ili katika hayo uweze kupigana vile vita vizuri;
Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa ajili ya ahadi ya uzima ulio katika Kristo Yesu;
Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa uweza wa Mungu;
Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.
Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.
na upendo, na subira; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
Bali wewe, uwe mwenye kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza huduma yako kwa ukamilifu.
na kwa Afia, dada yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako.
Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu;
Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
ili kwamba vizazi vya wana wa Israeli wapate kujua ili kuwafundisha vita, hasa wao ambao hawakujua vita kabla ya wakati ule;