Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




2 Samueli 7:11 - Swahili Revised Union Version

naam, kama ilivyokuwa tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Tena BWANA anakuambia ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

tangu wakati nilipowateua waamuzi juu ya watu wangu Israeli, nami nitakulinda kutokana na adui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Mwenyezi-Mungu nakutangazia kuwa nitakujengea nyumba.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

tangu wakati nilipowateua waamuzi juu ya watu wangu Israeli, nami nitakulinda kutokana na adui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Mwenyezi-Mungu nakutangazia kuwa nitakujengea nyumba.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

tangu wakati nilipowateua waamuzi juu ya watu wangu Israeli, nami nitakulinda kutokana na adui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Mwenyezi-Mungu nakutangazia kuwa nitakujengea nyumba.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

na kama walivyofanya tangu mwanzo wakati nilipowaweka viongozi juu ya watu wangu Israeli. Pia nitawapa amani mbele ya adui zenu wote. “ ‘Mwenyezi Mungu akuambia kwamba Mwenyezi Mungu mwenyewe atakujengea nyumba.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

na kama walivyofanya tangu mwanzo wakati nilipowaweka viongozi juu ya watu wangu Israeli. Pia nitawapa raha mbele ya adui zenu wote. “ ‘bwana akuambia kwamba bwana mwenyewe atakujengea nyumba.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

naam, kama ilivyokuwa tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Tena BWANA anakuambia ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.

Tazama sura
Tafsiri zingine



2 Samueli 7:11
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, mfalme alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo BWANA alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote,


Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Bwana MUNGU; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumishi wako, kwa miaka mingi inayokuja baadaye; na hayo kwa namna ya kibinadamu, Ee Bwana MUNGU.


Kwa kuwa wewe, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli umenifunulia mimi, mtumishi wako, ukisema, Nitakujengea nyumba; kwa hiyo mimi, mtumishi wako, nimepata ujasiri nikuombe ombi hili.


Tena itakuwa, ukiyasikia yote nitakayokuamuru, na kuenda katika njia zangu, na kutenda yaliyo mema machoni pangu, ili kuzishika amri zangu na hukumu zangu kama Daudi mtumishi wangu alivyotenda, basi, nitakuwa pamoja nawe, nitakujengea nyumba iliyo imara, kama nilivyomjengea Daudi, nami nitakupa wewe Israeli.


Basi kwa hiyo, BWANA aishivyo, aliyenithibitisha na kunikalisha katika kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, akanifanyia nyumba, kama alivyoahidi, hakika atauawa leo hivi Adonia.


na tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi wawatawale watu wangu Israeli, nami nitawashinda adui zako wote. Pamoja na hayo nakuambia, ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.


huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakiimarisha milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.


Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;


Adui zao wakawaonea, Wakatiishwa chini ya mkono wao.


BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure.


Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.


Ilikuwa kwa sababu wale wakunga walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.


Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.


ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,


Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya kulingana na yale yaliyo katika moyo wangu na katika akili yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele.


Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika BWANA atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya BWANA; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.