Daudi akaona uchungu kwa kuwa BWANA amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza hata leo.
2 Samueli 6:9 - Swahili Revised Union Version Naye Daudi akamwogopa BWANA siku ile; akasema, Litanijiaje sanduku la BWANA? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hiyo Daudi alimwogopa Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa litanijiaje sanduku la Mwenyezi-Mungu?” Biblia Habari Njema - BHND Siku hiyo Daudi alimwogopa Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa litanijiaje sanduku la Mwenyezi-Mungu?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hiyo Daudi alimwogopa Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa litanijiaje sanduku la Mwenyezi-Mungu?” Neno: Bibilia Takatifu Daudi akamwogopa Mwenyezi Mungu siku ile, akasema, “Ni jinsi gani Sanduku la Mwenyezi Mungu litakavyoweza kunijia?” Neno: Maandiko Matakatifu Daudi akamwogopa bwana siku ile, akasema, “Ni jinsi gani Sanduku la bwana litakavyoweza kunijia?” BIBLIA KISWAHILI Naye Daudi akamwogopa BWANA siku ile; akasema, Litanijiaje sanduku la BWANA? |
Daudi akaona uchungu kwa kuwa BWANA amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza hata leo.
Lakini Mungu je? Hakika atakaa juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!
Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.
basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.
Kama vile Sara alivyomtii Abrahamu, akamwita bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, pasipo kutishwa na hofu yoyote.
Nao watu wa Beth-shemeshi wakasema, Ni nani awezaye kusimama mbele za BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Naye atapanda kwenda kwa nani kutoka kwetu?