2 Samueli 3:33 - Swahili Revised Union Version Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema, Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme alimwombolezea Abneri akisema, “Je, ilikuwaje Abneri akafa kama mpumbavu? Biblia Habari Njema - BHND Mfalme alimwombolezea Abneri akisema, “Je, ilikuwaje Abneri akafa kama mpumbavu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme alimwombolezea Abneri akisema, “Je, ilikuwaje Abneri akafa kama mpumbavu? Neno: Bibilia Takatifu Mfalme akaimba ombolezo hili kwa ajili ya Abneri: “Je, ilipasa Abneri afe kama anavyokufa mpumbavu? Neno: Maandiko Matakatifu Mfalme akaimba ombolezo hili kwa ajili ya Abneri: “Je, ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu? BIBLIA KISWAHILI Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema, Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu? |
Mikono yako haikufungwa, Wala miguu yako haikutiwa pingu; Aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka. Na watu wote wakaongeza kumlilia.
Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.
Kama kware akusanyaye makinda asiyoyaangua, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya maisha yake itamtoka, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.
Hayo ndiyo maombolezo watakayoimba; binti za mataifa watayaimba; kwa hayo wataomboleza kwa ajili ya Misri, na kwa ajili ya watu wake umati wote, asema Bwana MUNGU.