Naye Daudi akatuma mtu akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?
2 Samueli 23:39 - Swahili Revised Union Version na Uria, Mhiti; idadi yao ilikuwa watu thelathini na saba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na Uria, Mhiti. Wote pamoja walikuwa mashujaa thelathini na saba. Biblia Habari Njema - BHND na Uria, Mhiti. Wote pamoja walikuwa mashujaa thelathini na saba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na Uria, Mhiti. Wote pamoja walikuwa mashujaa thelathini na saba. Neno: Bibilia Takatifu na Uria Mhiti. Jumla yao wote walikuwa watu thelathini na saba. Neno: Maandiko Matakatifu na Uria, Mhiti. Jumla yao wote walikuwa watu thelathini na saba. BIBLIA KISWAHILI na Uria, Mhiti; idadi yao ilikuwa watu thelathini na saba. |
Naye Daudi akatuma mtu akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?
Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa Waamoni.
kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa BWANA, wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, siku zote za maisha yake, isipokuwa kuhusu Uria, Mhiti.
Ndipo Daudi akajibu, akamwambia Ahimeleki, Mhiti, na Abishai, mwana wa Seruya, ndugu yake Yoabu, akisema, Ni nani atakayeshuka pamoja nami kwa Sauli kambini? Abishai akasema, Mimi nitashuka pamoja nawe.