Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
2 Samueli 22:45 - Swahili Revised Union Version Wageni walinijia wakinyenyekea; Mara tu waliposikia habari zangu, Walinitii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wageni walinijia wakinyenyekea, mara waliposikia habari zangu walinitii. Biblia Habari Njema - BHND Wageni walinijia wakinyenyekea, mara waliposikia habari zangu walinitii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wageni walinijia wakinyenyekea, mara waliposikia habari zangu walinitii. Neno: Bibilia Takatifu nao wageni huja wakininyenyekea, mara wanisikiapo, hunitii. Neno: Maandiko Matakatifu nao wageni huja wakininyenyekea, mara wanisikiapo, hunitii. BIBLIA KISWAHILI Wageni walinijia wakinyenyekea; Mara tu waliposikia habari zangu, Walinitii. |
Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
Wala mgeni, aambatanaye na BWANA, asiseme hivi, Hakika yake BWANA atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu.
Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;
Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.