nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
2 Samueli 22:36 - Swahili Revised Union Version Nawe umenipa ngao ya wokovu wako; Na unyenyekevu wako umenikuza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umenipa ngao yako ya kuniokoa; msaada wako umenifanya mkuu. Biblia Habari Njema - BHND Umenipa ngao yako ya kuniokoa; msaada wako umenifanya mkuu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umenipa ngao yako ya kuniokoa; msaada wako umenifanya mkuu. Neno: Bibilia Takatifu Hufanya msaada wa wokovu wako kuwa ngao yangu; msaada wako umeniinua niwe mkuu. Neno: Maandiko Matakatifu Hunipa ngao yako ya ushindi, unajishusha chini ili kuniinua. BIBLIA KISWAHILI Nawe umenipa ngao ya wokovu wako; Na unyenyekevu wako umenikuza. |
nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;
Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kulia umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.