2 Samueli 22:15 - Swahili Revised Union Version Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatimua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliwalenga adui mishale, akawatawanya, alirusha umeme, akawatimua. Biblia Habari Njema - BHND Aliwalenga adui mishale, akawatawanya, alirusha umeme, akawatimua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliwalenga adui mishale, akawatawanya, alirusha umeme, akawatimua. Neno: Bibilia Takatifu Aliipiga mishale na kutawanya adui, akawafukuza kwa umeme mkubwa wa radi. Neno: Maandiko Matakatifu Aliipiga mishale na kutawanya adui, umeme wa radi na kuwafukuza. BIBLIA KISWAHILI Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatimua. |
Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.
BWANA naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kukwelea kwenda Beth-horoni, na kuwapiga hadi kufikia Azeka, tena hadi kufikia Makeda.
Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; lakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli.