Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
2 Samueli 22:11 - Swahili Revised Union Version Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipanda kiumbe chenye mabawa na kuruka, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Biblia Habari Njema - BHND Alipanda kiumbe chenye mabawa na kuruka, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipanda kiumbe chenye mabawa na kuruka, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Neno: Bibilia Takatifu Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mabawa ya upepo. Neno: Maandiko Matakatifu Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo. BIBLIA KISWAHILI Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo. |
Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la BWANA wa majeshi akaaye juu ya makerubi.
Na kuziweka nguzo za ghorofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,
Magari ya Mungu ni elfu ishirini, maelfu kwa maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai, Katika patakatifu.
Wewe uchungaye Israeli, usikie, Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi; Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.
Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi yawe kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.
Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.
Basi wakatuma watu kwenda Shilo, nao wakalileta toka huko sanduku la Agano la BWANA wa majeshi, akaaye juu ya makerubi; na Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwako huko pamoja na sanduku la Agano la Mungu.