Ndipo wakatoka nyuma yake watu wa Yoabu, na Wakerethi na Wapelethi, na mashujaa wote; wakatoka Yerusalemu, ili kumfuatia Sheba, mwana wa Bikri.
2 Samueli 20:23 - Swahili Revised Union Version Basi Yoabu alikuwa akiongoza jeshi lote la Israeli; na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa akiwaongoza Wakerethi, na Wapelethi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa Yoabu alikuwa mkuu wa jeshi lote la Israeli. Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa mkuu wa Wakerethi na Wapelethi. Biblia Habari Njema - BHND Sasa Yoabu alikuwa mkuu wa jeshi lote la Israeli. Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa mkuu wa Wakerethi na Wapelethi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa Yoabu alikuwa mkuu wa jeshi lote la Israeli. Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa mkuu wa Wakerethi na Wapelethi. Neno: Bibilia Takatifu Yoabu alikuwa jemadari wa jeshi lote la Israeli; Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; Neno: Maandiko Matakatifu Yoabu alikuwa jemadari wa jeshi lote la Israeli; Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; BIBLIA KISWAHILI Basi Yoabu alikuwa akiongoza jeshi lote la Israeli; na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa akiwaongoza Wakerethi, na Wapelethi; |
Ndipo wakatoka nyuma yake watu wa Yoabu, na Wakerethi na Wapelethi, na mashujaa wote; wakatoka Yerusalemu, ili kumfuatia Sheba, mwana wa Bikri.
Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wawili wakali wa Moabu, pia aliingia katika shimo na kumwua simba wakati wa theluji;
Daudi akatawala juu ya Israeli wote; naye Daudi akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.
Akashauriana na Yoabu, mwana wa Seruya, na Abiathari, kuhani; nao wakamsaidia Adonia, wakamfuata.
Ila Sadoki, kuhani, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Nathani, nabii, na Shimei, na Rei, na mashujaa wa Daudi, hao hawakuwa pamoja na Adonia.
Hata mwaka wa saba Yehoyada akatuma, na kuwaleta wakuu wa mamia, wa Wakari, na wa walinzi, akawaleta kwake ndani ya nyumba ya BWANA; akapatana nao, akawaapisha nyumbani mwa BWANA, akawaonesha huyo mwana wa mfalme.