Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo.
2 Samueli 18:10 - Swahili Revised Union Version Basi mtu mmoja akaona hayo, akaenda akamwambia Yoabu, akasema, Tazama, mimi nilimwona Absalomu ametundikwa katika mwaloni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu fulani aliyeona tukio hilo, akamwambia Yoabu, “Nimemwona Absalomu akininginia kwenye mwaloni.” Biblia Habari Njema - BHND Mtu fulani aliyeona tukio hilo, akamwambia Yoabu, “Nimemwona Absalomu akininginia kwenye mwaloni.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu fulani aliyeona tukio hilo, akamwambia Yoabu, “Nimemwona Absalomu akining'inia kwenye mwaloni.” Neno: Bibilia Takatifu Mtu mmoja alipoona hivyo, akamwambia Yoabu, “Nimemwona Absalomu akining’inia kwenye mwaloni.” Neno: Maandiko Matakatifu Mmojawapo wa wale watu alipoona, akamwambia Yoabu, “Nimemwona Absalomu akining’inia kwenye mti wa mwaloni.” BIBLIA KISWAHILI Basi mtu mmoja akaona hayo, akaenda akamwambia Yoabu, akasema, Tazama, mimi nilimwona Absalomu ametundikwa katika mwaloni. |
Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo.
Naye Yoabu akamwambia mtu yule aliyempasha habari, Je! Wewe umeona haya; Mbona, basi, hukumpiga hadi chini papo hapo? Nami ningalikupa fedha kumi na mshipi.
Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.
basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za BWANA katika Gibeoni, katika mlima wa BWANA. Mfalme akasema, Nitawatoa.
Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;