2 Samueli 17:3 - Swahili Revised Union Version na hao watu wote nitawarejesha kwako; kama bibi arusi anavyorudi nyumbani kwa mumewe. Kurudi kwa yule mtu umtafutaye ni kana kurudi kwa wote; maana watu wote watakuwa katika amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na kuwarudisha watu wengine wote kwako kama bibiarusi anavyokwenda nyumbani kwa mumewe. Wewe unayatafuta maisha ya mtu mmoja tu; na watu wengine watakuwa na amani.” Biblia Habari Njema - BHND na kuwarudisha watu wengine wote kwako kama bibiarusi anavyokwenda nyumbani kwa mumewe. Wewe unayatafuta maisha ya mtu mmoja tu; na watu wengine watakuwa na amani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na kuwarudisha watu wengine wote kwako kama bibiarusi anavyokwenda nyumbani kwa mumewe. Wewe unayatafuta maisha ya mtu mmoja tu; na watu wengine watakuwa na amani.” Neno: Bibilia Takatifu na kuwarudisha watu wote kwako. Kifo cha mtu yule unayemtafuta kitamaanisha kurudi kwa wote, hakuna hata mtu mmoja atakayeumizwa.” Neno: Maandiko Matakatifu na kuwarudisha watu wote kwako. Kifo cha mtu yule unayemtafuta kitamaanisha kurudi kwa wote, hakuna hata mtu mmoja atakayeumizwa.” BIBLIA KISWAHILI na hao watu wote nitawarejesha kwako; kama bibi harusi anavyorudi nyumbani kwa mumewe. Kurudi kwa yule mtu umtafutaye ni kama kurudi kwa wote; maana watu wote watakuwa katika amani. |
Kisha Abneri akamwambia Daudi, Nitaondoka, niende zangu; nami nitamkusanyia bwana wangu mfalme Israeli wote, ili wafanye agano nawe, ukamiliki juu ya wote inaowatamani roho yako. Basi Daudi akamruhusu Abneri; naye akaenda zake kwa amani.
Wameliponya jeraha la watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.