Basi Daudi akamwambia yule mjumbe, Basi, mwambie Yoabu maneno haya, Jambo hili lisiwe baya machoni pako, maana upanga hula huyu kama unavyomla huyu; zidi kutia nguvu vita vyako juu ya mji ukauangushe; nawe mtie moyo.
2 Samueli 14:14 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa hatuna budi kufa, nasi tu kama maji yaliyomwagika chini, yasiyoweza kuzoleka tena; wala Mungu haondoi maisha ila hufikiri shauri, kwamba yeye aliyefukuzwa asiwe mkimbizi kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sisi sote lazima tutakufa. Sisi ni kama maji yaliyomwagika chini ambayo hayazoleki. Hata Mungu hafanyi tofauti kwa mtu huyu na tofauti kwa mwingine; yeye hutafuta njia ili waliopigwa marufuku, wakakimbia, wapate kurudi. Biblia Habari Njema - BHND Sisi sote lazima tutakufa. Sisi ni kama maji yaliyomwagika chini ambayo hayazoleki. Hata Mungu hafanyi tofauti kwa mtu huyu na tofauti kwa mwingine; yeye hutafuta njia ili waliopigwa marufuku, wakakimbia, wapate kurudi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sisi sote lazima tutakufa. Sisi ni kama maji yaliyomwagika chini ambayo hayazoleki. Hata Mungu hafanyi tofauti kwa mtu huyu na tofauti kwa mwingine; yeye hutafuta njia ili waliopigwa marufuku, wakakimbia, wapate kurudi. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile maji yaliyomwagika ardhini hayawezi kuzoleka, hivyo sisi kufa ni lazima. Lakini hivyo sivyo Mungu anataka; bali hupanga njia ili mtu aliyefukuzwa asibaki akiwa ametengwa naye. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile maji yaliyomwagika ardhini, yasivyoweza kuzoleka tena, hivyo sisi kufa ni lazima. Lakini Mungu haondoi uhai, badala yake, yeye hufanya njia ili kwamba aliyefukuzwa asibaki akiwa amefarikishwa naye. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa hatuna budi kufa, nasi tu kama maji yaliyomwagika chini, yasiyoweza kuzoleka tena; wala Mungu haondoi maisha ila hufikiri shauri, kwamba yeye aliyefukuzwa asiwe mkimbizi kwake. |
Basi Daudi akamwambia yule mjumbe, Basi, mwambie Yoabu maneno haya, Jambo hili lisiwe baya machoni pako, maana upanga hula huyu kama unavyomla huyu; zidi kutia nguvu vita vyako juu ya mji ukauangushe; nawe mtie moyo.
Hata sasa nilivyokuja mimi kunena neno hili na bwana wangu mfalme, ni kwa sababu watu wamenitisha; nami, mjakazi wako, nikasema, Mimi nitanena sasa kwa mfalme; labda itakuwa mfalme atanifanyia haja yangu mimi mtumishi wake.
Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za huduma yangu, Hadi kufunguliwa kwangu kunifikie.
Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, Niifikie nyumba waliyoaandaliwa wenye uhai wote.
Sembuse yeye huwajali nyuso za wakuu, Wala hawajali matajiri kuliko maskini? Kwani wote ni kazi ya mikono yake,
Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu.
Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti
Wamemwaga damu yao kama maji Pande zote za Yerusalemu, Wala hapakuwa na mtu wa kuwazika.
Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonesha mahali atakapopakimbilia.
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana tuzo tena; maana hata kumbukumbu lao limesahauliwa.
Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?
Nao wataukiri uovu wao, na uovu wa baba zao, katika maasi yao waliyoasi juu yangu, tena kwa kuwa wameendelea kunifanyia kinyume,
Miji hiyo sita itakuwa pa kukimbilia usalama kwa ajili ya wana wa Israeli, kwa ajili ya mgeni na kwa ajili ya aishiye nao kama mgeni; ili kila amwuaye mtu, bila kukusudia kuua, apate mahali pa kukimbilia.
nao mkutano utamwokoa yule aliyemwua mtu na mkono wa mwenye kulipiza kisasi cha damu; tena mkutano utamrejesha katika mji wake wa makimbilio, aliokuwa anaukimbilia; naye atakaa humo hata kifo chake kuhani mkuu, aliyepakwa mafuta matakatifu.
kwa sababu ilimpasa kukaa ndani ya mji wake wa makimbilio hadi kifo chake kuhani mkuu lakini kuhani mkuu atakapokwisha kufa huyo mwuaji atarudi aende nchi ya urithi wake.
Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, tunajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu.
Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea watu, wala kukubali rushwa.
Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.