Daudi akamwambia, Mambo yalikuwaje? Tafadhali niambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani, tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe, wamekufa.
2 Samueli 1:5 - Swahili Revised Union Version Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Daudi akamwuliza yule kijana, “Unajuaje kuwa Shauli na Yonathani mwanawe wamekufa?” Biblia Habari Njema - BHND Daudi akamwuliza yule kijana, “Unajuaje kuwa Shauli na Yonathani mwanawe wamekufa?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Daudi akamwuliza yule kijana, “Unajuaje kuwa Shauli na Yonathani mwanawe wamekufa?” Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamu vipi kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?” Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamuje kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?” BIBLIA KISWAHILI Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa? |
Daudi akamwambia, Mambo yalikuwaje? Tafadhali niambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani, tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe, wamekufa.
Yule kijana aliyempa habari akasema, Nilikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi.