2 Samueli 1:26 - Swahili Revised Union Version Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nasikitika kwa ajili yako, ndugu yangu Yonathani. Umekuwa kwangu daima mtu wa kupendeza, pendo lako kwangu limekuwa la ajabu, la ajabu kuliko la mwanamke. Biblia Habari Njema - BHND Nasikitika kwa ajili yako, ndugu yangu Yonathani. Umekuwa kwangu daima mtu wa kupendeza, pendo lako kwangu limekuwa la ajabu, la ajabu kuliko la mwanamke. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nasikitika kwa ajili yako, ndugu yangu Yonathani. Umekuwa kwangu daima mtu wa kupendeza, pendo lako kwangu limekuwa la ajabu, la ajabu kuliko la mwanamke. Neno: Bibilia Takatifu Nahuzunika kwa ajili yako, Yonathani ndugu yangu, kwangu ulikuwa mpendwa sana. Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, wa ajabu kuliko ule wa wanawake. Neno: Maandiko Matakatifu Nahuzunika kwa ajili yako, Yonathani ndugu yangu, kwangu ulikuwa mpendwa sana. Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, wa ajabu zaidi kuliko ule wa wanawake. BIBLIA KISWAHILI Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake. |
Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
Lakini huyo Yonathani, mwana wake Sauli, alikuwa akipendezwa sana na Daudi. Basi Yonathani akamwambia Daudi, akasema, Sauli, baba yangu, anakusudia kukuua; basi, nakusihi, ujiangalie sana asubuhi, ukae mahali pa siri na kujificha;
Naye Yonathani akamwapisha Daudi mara ya pili, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake; kwa maana alimpenda kama alivyoipenda roho yake mwenyewe.
Basi mara alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana, wakaliliana, hata Daudi akazidi.
Ndipo Yonathani, mwana wa Sauli, akainuka akamwendea Daudi huko Horeshi, akamtia nguvu mkono wake katika Mungu.