Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
1 Wakorintho 2:16 - Swahili Revised Union Version Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maandiko yasema: “Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?” Lakini sisi tunayo akili ya Kristo. Biblia Habari Njema - BHND Maandiko yasema: “Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?” Lakini sisi tunayo akili ya Kristo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maandiko yasema: “Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?” Lakini sisi tunayo akili ya Kristo. Neno: Bibilia Takatifu “Kwa maana ni nani aliyefahamu mawazo ya Mwenyezi Mungu ili apate kumfundisha?” Lakini sisi tunayo mawazo ya Al-Masihi. Neno: Maandiko Matakatifu “Kwa maana ni nani aliyefahamu mawazo ya Bwana Isa ili apate kumfundisha?” Lakini sisi tunayo mawazo ya Al-Masihi. BIBLIA KISWAHILI Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. |
Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la BWANA, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia?
Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;