Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.
1 Wafalme 2:23 - Swahili Revised Union Version Ndipo mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, isipokuwa Adonia amenena neno hili juu ya uhai wake mwenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo mfalme Solomoni akaapa kwa jina la Mwenyezi-Mungu, akisema, “Mungu na aniulie mbali ikiwa Adoniya hatakufa kwa sababu ya kutoa ombi hili! Biblia Habari Njema - BHND Hapo mfalme Solomoni akaapa kwa jina la Mwenyezi-Mungu, akisema, “Mungu na aniulie mbali ikiwa Adoniya hatakufa kwa sababu ya kutoa ombi hili! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo mfalme Solomoni akaapa kwa jina la Mwenyezi-Mungu, akisema, “Mungu na aniulie mbali ikiwa Adoniya hatakufa kwa sababu ya kutoa ombi hili! Neno: Bibilia Takatifu Mfalme Sulemani akaapa kwa Mwenyezi Mungu, akasema: “Mungu na aniadhibu vikali zaidi ikiwa Adoniya hatalipa kwa uhai wake kwa ajili ya ombi hili! Neno: Maandiko Matakatifu Mfalme Sulemani akaapa kwa bwana, akasema: “Mungu na aniulie mbali, tena bila huruma, ikiwa Adoniya hatalipa kwa uhai wake kwa ajili ya ombi hili! BIBLIA KISWAHILI Ndipo mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, isipokuwa Adonia amenena neno hili juu ya uhai wake mwenyewe. |
Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.
Wakaja na watu wote wamshurutishe Daudi kula chakula, kukiwa bado mchana; lakini Daudi akaapa, akasema Mungu anitendee vivyo hivyo, na kuzidi, nikionja mkate, au kingine chochote kabla ya jua kutua.
Mungu amfanyie Abneri vivyo hivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile BWANA alivyomwapia;
Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.
Ndipo Ben-hadadi akatuma kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu.
Ndipo akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, kikimbakia kichwa Elisha mwana wa Shafati juu yake leo.
Kwa ajili ya ulimi wao wataangamizwa; Wote wawaonao watatetemeka kwa hofu. Wote wawaonao watatikisa kichwa.
Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.
Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, nichukuaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
Pale utakapofia ndipo nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; BWANA anitende vivyo hivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.
Naye Sauli akasema, Mungu anifanyie hivi, na kuzidi; kwa kuwa hakika utakufa, Yonathani.