Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, na unakwenda wapi? Akanena, Namkimbia bimkubwa wangu Sarai.
1 Wafalme 19:9 - Swahili Revised Union Version Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la BWANA likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huko, akafika penye pango, akakaa humo. Mara neno la Mwenyezi-Mungu likamjia: “Elia! Unafanya nini hapa?” Biblia Habari Njema - BHND Huko, akafika penye pango, akakaa humo. Mara neno la Mwenyezi-Mungu likamjia: “Elia! Unafanya nini hapa?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huko, akafika penye pango, akakaa humo. Mara neno la Mwenyezi-Mungu likamjia: “Elia! Unafanya nini hapa?” Neno: Bibilia Takatifu Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule. Nalo neno la Mwenyezi Mungu likamjia, kusema, “Unafanya nini hapa, Ilya?” Neno: Maandiko Matakatifu Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule. Nalo neno la bwana likamjia, kusema, “Unafanya nini hapa, Ilya?” BIBLIA KISWAHILI Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la BWANA likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? |
Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, na unakwenda wapi? Akanena, Namkimbia bimkubwa wangu Sarai.
Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya?
Na sasa una nini utakayofaidi katika njia iendayo Misri, kunywa maji ya Shihori? Au una nini utakayofaidi katika njia iendayo Ashuru, kunywa maji ya ule Mto?
Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.
Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajitengenezea kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hadi aone mji ule utakuwaje.
(watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizungukazunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.