mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
1 Timotheo 5:7 - Swahili Revised Union Version Mambo hayo pia uyaagize, ili wasiwe na lawama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wape maagizo haya, wasije wakawa na lawama. Biblia Habari Njema - BHND Wape maagizo haya, wasije wakawa na lawama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wape maagizo haya, wasije wakawa na lawama. Neno: Bibilia Takatifu Wape watu maagizo haya pia, ili asiwepo yeyote wa kulaumiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Wape watu maagizo haya pia, ili asiwepo yeyote wa kulaumiwa. BIBLIA KISWAHILI Mambo hayo pia uyaagize, ili wasiwe na lawama. |
mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;
Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani;