Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
1 Timotheo 5:3 - Swahili Revised Union Version Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli. Biblia Habari Njema - BHND Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli. Neno: Bibilia Takatifu Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli. Neno: Maandiko Matakatifu Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli. BIBLIA KISWAHILI Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli. |
Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
BWANA huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huiharibu.
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Waache watoto wako wasio na baba, mimi nitawahifadhi hai, na wajane wako na wanitumaini mimi.
basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.
Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wengi mjini walikuwa pamoja naye.
Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.
Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kigiriki juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.
Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu ghorofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.
Akampa mkono, akamwinua; hata kisha akawaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, akiwa hai.
Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.
na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
nawe utafurahi mbele ya BWANA, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake.
nawe utafurahi katika sikukuu yako, wewe, na mwanao, na binti yako, na mtumwa wako, na mjakazi wako, na Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako.
Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.
Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine, ingawa tungeweza kuwalemea kama Mitume wa Kristo;
Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.