Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji wakati wa jioni, wakati ambapo wanawake wanakwenda kuteka maji.
1 Samueli 9:11 - Swahili Revised Union Version Walipokuwa wakikwea mjini, wakakutana na wasichana, waliokuwa wakienda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walipokuwa wanapanda mlima kuelekea mjini, wakakutana na wasichana waliokuwa wakienda kuteka maji. Wakawauliza wasichana hao, “Je, mwonaji yuko mjini?” Biblia Habari Njema - BHND Walipokuwa wanapanda mlima kuelekea mjini, wakakutana na wasichana waliokuwa wakienda kuteka maji. Wakawauliza wasichana hao, “Je, mwonaji yuko mjini?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walipokuwa wanapanda mlima kuelekea mjini, wakakutana na wasichana waliokuwa wakienda kuteka maji. Wakawauliza wasichana hao, “Je, mwonaji yuko mjini?” Neno: Bibilia Takatifu Walipokuwa wakipanda mlima kwenda mjini, wakakutana na baadhi ya wasichana wakikuja kuchota maji, nao wakawauliza, “Je, mwonaji yuko?” Neno: Maandiko Matakatifu Walipokuwa wakipanda mlima kwenda mjini, wakakutana na baadhi ya wasichana wanakuja kuchota maji, nao wakawauliza, “Je, mwonaji yuko?” BIBLIA KISWAHILI Walipokuwa wakikwea mjini, wakakutana na wasichana, waliokuwa wakienda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko? |
Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji wakati wa jioni, wakati ambapo wanawake wanakwenda kuteka maji.
Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Abrahamu, naye ana mtungi begani pake.
Wakasema, Hatuwezi, Mpaka makundi yote yakusanyike, watu wakabingirishe jiwe katika kinywa cha kisima, ndipo tunapowanywesha kondoo.
Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.
Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji, Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA; Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli. Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni.
Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu.