ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
1 Samueli 8:1 - Swahili Revised Union Version Na Samweli alipozeeka, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Samueli alipokuwa mzee, aliwafanya watoto wake wa kiume kuwa waamuzi wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Samueli alipokuwa mzee, aliwafanya watoto wake wa kiume kuwa waamuzi wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Samueli alipokuwa mzee, aliwafanya watoto wake wa kiume kuwa waamuzi wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli. BIBLIA KISWAHILI Hata Samweli alipozeeka, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli. |
ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lolote kwa upendeleo.
Huyo alikuwa na watoto wa kiume thelathini waliokuwa wakipanda wanapunda thelathini, nao walikuwa na miji thelathini, ambayo inaitwa Hawoth-yairi hata hivi leo, nayo iko katika nchi ya Gileadi.
Naye alikuwa na wana arubaini, na wajukuu thelathini, waliokuwa wakipanda wanapunda sabini; akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka minane.
Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe, Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani, Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu.
Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo.