Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




1 Samueli 7:9 - Swahili Revised Union Version

Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli; BWANA akamwitikia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kwa hiyo Samueli alichukua mwanakondoo anayenyonya akamtolea Mwenyezi-Mungu kama sadaka ya kuteketezwa nzima. Kisha Samueli akamlilia Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya Israeli, naye akajibu kilio chake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kwa hiyo Samueli alichukua mwanakondoo anayenyonya akamtolea Mwenyezi-Mungu kama sadaka ya kuteketezwa nzima. Kisha Samueli akamlilia Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya Israeli, naye akajibu kilio chake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kwa hiyo Samueli alichukua mwanakondoo anayenyonya akamtolea Mwenyezi-Mungu kama sadaka ya kuteketezwa nzima. Kisha Samueli akamlilia Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya Israeli, naye akajibu kilio chake.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kisha Samweli akamchukua mwana-kondoo anyonyaye na kumtoa mzima kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu. Akamlilia Mwenyezi Mungu kwa niaba ya Israeli, naye Mwenyezi Mungu akamjibu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kisha Samweli akamchukua mwana-kondoo anyonyaye na kumtoa mzima kama sadaka ya kuteketezwa kwa bwana. Akamlilia bwana kwa niaba ya Israeli, naye bwana akamjibu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli; BWANA akamwitikia.

Tazama sura
Tafsiri zingine



1 Samueli 7:9
16 Marejeleo ya Msalaba  

Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Musa na Haruni walikuwa makuhani wake, Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake, Walimlilia BWANA naye akawaitikia;


Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.


Hapo ng'ombe, kondoo au mbuzi, akizaliwa, atakuwa pamoja na mamaye muda wa siku saba; na siku ya nane na baadaye atakubaliwa kuwa ni sadaka ya kutolewa kwa BWANA kwa njia ya moto.


Nikamwomba BWANA, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu.


Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.


ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.


Hata wakazi wa mji walipoamka asubuhi na mapema, wakaona madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa.


Nawe utateremka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakuteremkia huko, ili kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja, hata nitakapokujia, na kukuonesha yatakayokupasa kuyafanya.


Je! Leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba atume ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu mlioufanya machoni pa BWANA, ni mwingi sana, kwa kujitakia mfalme.


Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi BWANA akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea BWANA dhabihu.


Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya kulingana na yale yaliyo katika moyo wangu na katika akili yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele.


Kisha alikuwa akirudi Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Waisraeli; na huko akamjengea BWANA madhabahu.


Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu;