Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 7:8 - Swahili Revised Union Version

8 Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, Usiache kumlilia BWANA, Mungu wetu, kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Basi, wakamwambia Samueli, “Usiache kumlilia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwa ajili yetu. Endelea kumlilia atuokoe kutoka kwa Wafilisti.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Basi, wakamwambia Samueli, “Usiache kumlilia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwa ajili yetu. Endelea kumlilia atuokoe kutoka kwa Wafilisti.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Basi, wakamwambia Samueli, “Usiache kumlilia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwa ajili yetu. Endelea kumlilia atuokoe kutoka kwa Wafilisti.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Wakamwambia Samweli, “Usiache kumlilia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa ajili yetu, ili apate kutuokoa na mikono ya Wafilisti.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Wakamwambia Samweli, “Usiache kumlilia bwana, Mungu wetu, kwa ajili yetu, ili apate kutuokoa na mikono ya Wafilisti.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, Usiache kumlilia BWANA, Mungu wetu, kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 7:8
7 Marejeleo ya Msalaba  

Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo kamanda ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na BWANA, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.

Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.

Lakini ikiwa hao ni manabii, na ikiwa neno la BWANA liko kwao, basi na wamwombe BWANA wa majeshi, kwamba vyombo vile vilivyosalia katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu, visiende Babeli.

wakamwambia Yeremia, nabii, Twakusihi, maombi yetu yakubaliwe mbele yako, ukatuombee kwa BWANA, Mungu wako, yaani, watu hawa wote waliosalia; maana tumesalia wachache tu katika watu wengi, kama macho yako yatuonavyo;

Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo