Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




1 Samueli 6:2 - Swahili Revised Union Version

Nao Wafilisti wakawaita makuhani na waaguzi, wakasema, Tulifanyieje sanduku la BWANA? Tuonesheni jinsi tuwezavyo kulirudisha mahali pake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Wafilisti waliwaita makuhani na waaguzi wao na kuwauliza, “Tufanyeje na sanduku hili la Mwenyezi-Mungu? Tuambieni namna gani tunavyoweza kulirudisha mahali pake.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Wafilisti waliwaita makuhani na waaguzi wao na kuwauliza, “Tufanyeje na sanduku hili la Mwenyezi-Mungu? Tuambieni namna gani tunavyoweza kulirudisha mahali pake.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Wafilisti waliwaita makuhani na waaguzi wao na kuwauliza, “Tufanyeje na sanduku hili la Mwenyezi-Mungu? Tuambieni namna gani tunavyoweza kulirudisha mahali pake.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wafilisti waliwaita makuhani wa Dagoni na waaguzi, na kuwaambia, “Tutafanya nini na hili Sanduku la Mwenyezi Mungu? Tuambieni jinsi tutakavyolirudisha mahali pake.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wafilisti waliwaita makuhani wa Dagoni na waaguzi, na kuwaambia, “Tutafanya nini na hili Sanduku la bwana? Tuambieni jinsi tutakavyolirudisha mahali pake.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nao Wafilisti wakawaita makuhani na waaguzi, wakasema, Tulifanyieje sanduku la BWANA? Tuonyesheni jinsi tuwezavyo kulirudisha mahali pake.

Tazama sura
Tafsiri zingine



1 Samueli 6:2
10 Marejeleo ya Msalaba  

Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.


Ndipo Farao naye akawaita wajuzi na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo hivyo kwa uganga wao.


Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapeana mikono na wana wa wageni.


Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na walozi, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme.


Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme.


Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?


Basi wakatuma watu waende kuwakusanya kwao wakuu wote wa Wafilisti, wakasema, Tulifanyieje sanduku la Mungu wa Israeli? Nao wakajibu, Sanduku la Mungu wa Israeli na lihamishwe liende Gathi. Wakalihamisha sanduku la Mungu wa Israeli.


Basi, hilo sanduku la BWANA lilikuwamo katika nchi ya Wafilisti muda wa miezi saba.