Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakarukaruka juu ya madhabahu waliyoifanya.
1 Samueli 5:3 - Swahili Revised Union Version Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kesho yake asubuhi, watu wa mji wa Ashdodi walipoamka waliona sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mungu. Wakaisimamisha tena sanamu ya Dagoni na kuiweka tena mahali pake. Biblia Habari Njema - BHND Kesho yake asubuhi, watu wa mji wa Ashdodi walipoamka waliona sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mungu. Wakaisimamisha tena sanamu ya Dagoni na kuiweka tena mahali pake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kesho yake asubuhi, watu wa mji wa Ashdodi walipoamka waliona sanamu ya Dagoni imeanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Mungu. Wakaisimamisha tena sanamu ya Dagoni na kuiweka tena mahali pake. Neno: Bibilia Takatifu Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la bwana! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake. BIBLIA KISWAHILI Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena. |
Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakarukaruka juu ya madhabahu waliyoifanya.
Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.
Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.
Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi stadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.
Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike.
Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa kutoka kwa taabu yake.
Lakini wote pia huwa kama wanyama, ni wapumbavu. Haya ni maelezo ya sanamu, ni shina la mti tu.
BWANA atakuwa wa kutisha sana kwao; kwa maana atawaua kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.
Na pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.
Kwa hiyo mtafanya sanamu za majipu yenu, na sanamu za panya wenu wanaoiharibu nchi; nanyi mtamtukuza huyo Mungu wa Israeli; huenda ataupunguza uzito wa mkono wake juu yenu, na juu ya miungu yenu, na juu ya nchi yenu.