Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Samueli 27:11 - Swahili Revised Union Version

Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Daudi hakumwacha mtu yeyote hai awe mwanamume au mwanamke ili aletwe Gathi; alifikiri moyoni: “Wanaweza wakaeleza juu yetu na kusema, ‘Daudi alifanya kitendo hiki na kile.’” Hivyo ndivyo Daudi alivyozoea kutenda wakati wote alipoishi katika nchi ya Wafilisti.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Daudi hakumwacha mtu yeyote hai awe mwanamume au mwanamke ili aletwe Gathi; alifikiri moyoni: “Wanaweza wakaeleza juu yetu na kusema, ‘Daudi alifanya kitendo hiki na kile.’” Hivyo ndivyo Daudi alivyozoea kutenda wakati wote alipoishi katika nchi ya Wafilisti.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Daudi hakumwacha hai mwanaume au mwanamke ili apate kuletwa Gathi, kwa maana aliwaza, “Wanaweza kujulisha habari zetu na kusema, ‘Hivi ndivyo alivyofanya Daudi.’ ” Hii ndiyo ilikuwa desturi yake wakati wote aliishi katika nchi ya Wafilisti.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Daudi hakumwacha hai mwanaume au mwanamke ili apate kuletwa Gathi, kwa maana Daudi aliwaza, “Wanaweza kujulisha habari zetu na kusema, ‘Hivi ndivyo alivyofanya Daudi.’ ” Hii ndiyo ilikuwa desturi yake wakati wote aliishi katika nchi ya Wafilisti.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Samueli 27:11
7 Marejeleo ya Msalaba  

Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.

Ikawa siku ya pili baada ya kumwua Gedalia, wala hapakuwa na mtu aliyejua habari hii,

Daudi akamwambia Abiathari, Siku ile alipokuwako Doegi, Mwedomi, nilijua hakika ya kuwa atamwambia Sauli; mimi nimewapatia watu wote wa jamaa ya baba yako kifo.

Naye Akishi alipomwuliza, Je! Mmeshambulia upande gani leo? Na Daudi akasema, Juu ya Negebu ya Yuda, au, juu ya Negebu ya Wayerameeli, au, juu ya Negebu ya Wakeni.

Hivyo Akishi akamsadiki Daudi, akasema, Amewachukiza kabisa hao watu wake Israeli; kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu hata milele.

nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wowote, ila wakawachukua, wakaenda zao.