Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.
1 Samueli 20:23 - Swahili Revised Union Version Na kwa habari ya neno lile tulilonena, wewe na mimi, angalia BWANA yu kati ya wewe na mimi milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kulingana na ahadi tulizowekeana, Mwenyezi-Mungu atakuwa shahidi kati yetu milele.” Biblia Habari Njema - BHND Kulingana na ahadi tulizowekeana, Mwenyezi-Mungu atakuwa shahidi kati yetu milele.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kulingana na ahadi tulizowekeana, Mwenyezi-Mungu atakuwa shahidi kati yetu milele.” Neno: Bibilia Takatifu Kuhusu yale tuliyozungumza wewe na mimi: kumbuka, Mwenyezi Mungu ndiye shahidi kati yako wewe na mimi milele.” Neno: Maandiko Matakatifu Kuhusu yale tuliyozungumza wewe na mimi: kumbuka, bwana ndiye shahidi kati yako wewe na mimi milele.” BIBLIA KISWAHILI Na kwa habari ya neno lile tulilonena, wewe na mimi, angalia BWANA yu kati ya wewe na mimi milele. |
Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.
Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe.
Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu. Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake.
Naye Yonathani akamwambia Daudi, Nenda kwa amani; kwa maana sisi sote wawili tumeapiana kwa jina la BWANA ya kwamba, BWANA atakuwa kati ya mimi na wewe, na kati ya uzao wangu na uzao wako milele. Daudi akaondoka, akaenda zake; Yonathani naye akaenda zake mjini.